KLABU ya Ken Gold ya Mbeya leo imekataa kuachia pointi zote baada ya kulazimisha sare ya bao 1-1 dhidi Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Katika kipute hicho kilichofanyika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya bao la kusawazisha la Ken Gold limefungwa na Emmanuel Mpuka dakika 87 baada ya Coastal Union kutangulia kupata goli dakika ya 46 lililofungwa na Abdallah Hassan.