ICC kujadili waranti wanazotoa

UHOLANZI : NCHI wanachama wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC, wamekutana katika mkutano wa 23 ambapo watachagua kamati mpya na kupitisha bajeti ya mahakama hiyo ya ICC.
Katika mkutano huo, wawakilishi wa nchi 124 ambao ni wanachama wa ICC watajumuika mjini The Hague Uholanzi kuanzia tarehe 2 Desemba hadi tarehe 7 Desemba .
ICC ilianzishwa mwaka 2002 na imekuwa kimbilio la mwisho la kuwafungulia mashitaka watu waliohusika na ukatili, uhalifu wa kivita, uhalifu dhidi ya binadamu na mauaji ya kimbari.
Mahakama hiyo huanzisha kesi pale mataifa husika yasipokuwa na uwezo au kutoonyesha utayari wa kushtaki vitendo vya uhalifu kwenye maeneo yao.
Mkutano huu unajiri wakati mahakama hiyo ikikabiliwa na shinikizo la kufuta uamuzi wake wa kutoa waranti wa kukamatwa kwa maafisa wa Israel na kiongozi wa Hamas.



