Idadi watu waliokufa maporomoko Uganda yafikia 28

UGANDA : WATU wapatao 28 wamekufa nchini Uganda kufuatia maporomoko ya ardhi yaliyotokea wiki iliyopita.
Maporomoko hayo yalivikumba vijiji kadhaa huku mamia ya watu bado hawajulikani walipo.
Zaidi ya watu 100 wanahofiwa kupotea, kwenye miteremko ya Mlima Elgon, kwenye mpaka na Kenya, yapata kilomita 300 (maili 190) mashariki mwa mji mkuu wa Kampala.
Tangu Oktoba mwaka huu mvua kubwa zimeendelea kunyesha na kusababisha mafuriko na maporomoko ya ardhi katika baadhi ya maeneo ya Uganda.
Eneo lililo limekumbwa na maporomoko ya udongo yaliyosababisha vifo vya watu wengi mwaka 2010, takribani watu 80 walikufa. SOMA: Uganda yapewa mkopo dola miiioni 600
Hatahivyo, juhudi za serikali za kuwaondoa wakaazi katika maeneo yanayokumbwa na majanga nchini humo bado hazijaweza kuzaa matunda kutokana na wakaazi wengi nimasikini na hawana uwezo wa kuhamia maeneo mengine.



