Watembeleaji makumbusho ya taifa waongezeka

DAR ES SALAAM :Idadi ya watu wanaotembelea Makumbusho ya Taifa imeongezeka kutoka 500,000 mwaka 2019 hadi 800,000 mwaka huu.
Mkurugenzi wa Makumbusho ya Taifa, Dk.Noel Lwoga amesema ili kumuenzi mwasisi wa taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere watanzania wanapaswa kutembelea vivutio vilivyopo katika makumbusho hayo ili kuweza kujua historia.

Noel amesema ongezeko hilo la utalii limechangiwa na Rais Samia kwa kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini, programu mbalimbali walizoziweka kitengo chao cha masoko, matukio ambayo makumbusho inayoyabuni katika vituo vyake na mali kale, pamoja na mabalozi .
Muhifadhi Kiongozi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni, Agness Robert amesema kazi yao makumbusho ya Taifa ni kufanya tafiti, programu na maonesho mbalimbali na kutoa elimu kwa jamii kuhusiana na urithi wa utamaduni na asili.

Kwa upande wao wanafunzi waliotembelea makumbusho hayo Bariki Mtawa Rais wa Serikali ya Wanafunzi Chuo cha Kumbumbukumbu ya Mwalimu Nyerere na Clara Joseph Mwanafunzi Chuo cha Mwalimu Nyerere wamesema makumbusho hayo na vivutio na historia iliyopo kwenye makumbusho ya Taifa vitawapa elimu mbalimbali



