Mawaziri wako kazini kuimarisha usalama

SYRIA : WAZIRI Mkuu wa Syria, Mohammed Ghazi Jalali amesema mawaziri kadhaa bado wanafanya kazi mjini Damascus hata baada ya waasi kuuteka mji mkuu na kumpindua Rais Bashar al Assad.

Waziri Mkuu  Ghazi amebakia katika wadhifa wake ili kuhakikisha  usalama wa nchi unaimarika katika kipindi hiki cha  serikali ya mpito.

Hatahivyo amesema serikali inawasiliana na waasi na  yuko tayari kukutana na kiongozi wa waasi , Abu Mohammed al-Golani kwa lengo la kujadili mustakbali wa nchi.  SOMA: Kesi ya Septemba 11 kunguruma wiki ijayo

Wakatihuohuo, misururu ya wakimbizi waliovuka kutoka nchi jirani na kuingia Syria wameamua kurejea nyumbani  huku wakiwa na matumaini makubwa ya amani nchini humo.

Kiongozi wa waasi, Abu Mohammed al -Golani aliyekuwa mpiganaji wa kundi la kigaidi la al- Qaeda ambaye baadaye alijitenga na kundi hilo ameahidi kuleta serikali wakilishi itakayofuata misingi ya kidini.

Habari Zifananazo

Back to top button