SOMALIA: Viongozi wa Jubaland bado wanapigana na jeshi

SOMALIA : MAPIGANO yamezuka tena kati ya vikosi kutoka jimbo la Jubaland lenye utawala wake nchini Somalia na vikosi vya kijeshi.

Akizungumza na vyombo vya habari mjini Mogadishu nchini Somalia, naibu waziri wa usalama wa Jubaland Adan Ahmed Haji amesema mapigano hayo yanaonesha kutanuka kwa mivutano ya kisiasa katika eneo hilo.

Mwishoni mwa mwezi Novemba jimbo hilo linalopakana na Kenya na Ethiopia lilimrudisha tena madarakani rais wake Ahmed Islam Madobe kwa muhula wa tatu.

SOMA: Somalia rasmi mwanachama EAC

Habari Zifananazo

Back to top button