Halmashauri kufuatilia huduma za chanjo Mtwara

SERIKALI imekabidhi magari matano na pikipiki tisa kwa halmashauri zote tisa zilizopo mkoani Mtwara kwa ajili kufatilia usimamizi wa utoaji wa huduma za chanjo mkoni humo.
Akizungumza leo mkoani Mtwara wakati wa ghafla fupi ya kukabidhi magari na pikipiki hizo, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Patrick Sawala amesema anaendelea kutambua mchango mkubwa unaofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita kwa kuhakikisha mkoa na halmashauri zao zinaendelea kupata vitendea.
‘’Huduma za chanjo sote tunatambua ni muhimu katika kukinga jamii dhidi ya magonjwa mbalimbali yakiwemo ya surua, pepopunda, kifaduro na dondakoo ambayo miaka ya nyuma yalisababisha vifo vingi vya watoto wenye umri chini ya miaka mitato,’’amesema Sawala
Ajio wa magari hayo matano na pikipiki hizo tisa kunaenda kuimarisha huduma hizo kupitia ufatiliaji wa karibu wa huduma za chanjo kwenye vituo vya kutolea kuduma za afya pamoja na usambazaji wa chanjo zenyewe.

Aidha, wanaowajibu wa kuvitumia vyombo hivyo kuleta matokeo yaliyokusudiwa kuwafikia watoto zaidi ya elfu 70, wajawazito zaidi ya elfu 73 na wasichana wenye umri kati ya miaka 9 mpaka 14 watakaopata chanjo hiyo ili kuzuia saratani ya shingo ya kizazi zaidi ya 20 elfu kwa mwaka.
Akizungumza kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Mtwara, Nanjiva Nzunda amesema mkoa huo ni miongoni mwa mikoa iliyopokea magari na pikipiki kwa ajili ya usimamizi na uboreshaji wa huduma hiyo.
Magari hayo ikiwemo lori moja lililotolewa kuiwezesha ofisi ya mkuu wa mkoa huo kusambaza chanjo kwenye halmashauri na magari mengine manne haina ya Hilux yaliyotolewa katika halmashauri nne mkoani humo.
Halmashauri zilizopatiwa magari hayo ikiwemo Manispaa ya Mtwara Mikindani, Halmashauri ya Wilaya ya Masasi, Halmashauri ya Mji Nanyamba na Halmashauri ya Mji Newala hivyo mkoa una jumla ya halmashauri nane zenye magari ya usimamizi wa huduama hiyo yanayofanya kazi na halmashauri pekee itayobaki bila gari ni halmashauri ya Wilaya ya Newala.

Pia pikipiki hizo tisa zilimetolewa kwa ajili ya halmashauri zote tisa mbapo kila halmashauri itapatiwa pikipiki moja kwahiyo ni imani yake kuwa vyombo hivyo vitaongeza kasi ya kusimamia huduma za chanjo zinazotolewa katika halmashauri kupitia vituo 287 vya kutolea huduma za afya hatimaye kuwafikia walengwa wa chanjo 70,561 katika mkoa kwa zaidi ya asilimia 95.
Meya wa Manispaa ya Mtwara Mikindani, Shadida Ndile amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwaona watu wa mtwara kuhakikisha hasa kwenye sekta hiyo ya afya wanaendelea kuwa salama.



