ZEC yakamilisha maandalizi ya kura ya mapema

TUME ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) imethibitisha kukamilika kwa maandalizi ya kura ya mapema inayoanza leo Oktoba 28, 2025, ambapo baadhi ya maafisa wa ulinzi na usalama pamoja na watendaji wa tume watapiga kura katika vituo 50 Unguja na Pemba.

Akizungumza katika kikao na waangalizi wa uchaguzi wa ndani na nje kilichofanyika Makao Makuu ya ZEC Maisara, Mwenyekiti wa Tume, Jaji George Joseph Kazi, alisema vifaa vyote vya kupigia kura vimewasilishwa katika ofisi za wilaya tayari kwa zoezi hilo.

“Mandalizi yote yamekamilika. Kura ya mapema ni kwa mujibu wa sheria, na inalenga kurahisisha ushiriki wa watumishi wanaohusika na usimamizi wa uchaguzi siku ya Oktoba 29,” alisema Jaji Kazi. SOMA: ZEC : Maandalizi ya uchaguzi yakamilika

Wangalizi kutoka mashirika ya ndani na nje katika mkutano na maafisa wa tume ya Uchagizi Zanzibar (ZEC) chini ya uongozi wa mwenyekiti Jaji George Joseph Kazi, katika jengo la tume Maisara Oktoba 27, 2025 ambapo wangalizi wametakiwa kutoingilia kazi za tume, na wafuate sheria na muongozo wa uangalizi.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button