Adau aahidi maendeleo michezo kanda ya ziwa

MDAU wa michezo kutoka Manispaa ya Shinyanga, Mhandisi Jumbe James amesema yuko tayari kuendeleza michezo mbalimbali kwa kushirikisha na mikoa jirani Kanda ya Ziwa.

Mhandisi Jumbe amesema hayo katika zoezi la kukabidhi zawadi kwa washindi wa Bonanza la Dk Samia Jumbe Holiday kama alivyoahidi lililokuwa maalum kwa kuukaribisha mwaka 2025 kwenye Uwanja wa CCM Kambarage Mjini Shinyanga.

Mhandisi  Jumbe amesema Mkoa wa Shinyanga unatakiwa kuchangamka kimchezo kama maeneo mengine hivyo kupitia bonanza hili ameona mchezo wa kikapu (netboli) upatiwe siku yake maalum kwaajili ya mashindano.

Mchezo uliokuwa umevutia zaidi ni mbio za baiskeli ambapo washindani walikuwa zaidi ya 100 na kugawanywa katika makundi manne kwa ujumla zilitolewa Sh milioni 2,100,000 kwa washindi pekee.

Aidha wachezaji katika bonanza hilo kwa upande wa mpira miguu Timu ya Ngokolo ilijinyakulia zawadi  ya Sh 500,000 ngo’mbe mmoja, mchele kilo 100 na kreti saba za soda iliyokuwa ikicheza na  Rangers  ambayo nayo ilipata Sh 300,000 ngo’mbe mmoja, mchele kilo 100 na kreti ya soda.

Timu ya mpira wa miguu ya Upongoji Derby  na Upongoji Star  zilijinyakulia zawadi  ya Sh  milioni 1 Ngo’mbe mmoja ,mchele  kilo 100 na kreti saba za soda iliyokuwa ikicheza na  Upongoji  ambayo nayo ilipata Sh 300,000 ngo’mbe mmoja mchele kilo 100 na kreti saba za soda.

Kwa mpira miguu Timu ya  Bajaji ilijinyakulia zawadi  ya Sh 500,000 ngo’mbe mmoja, mchele  kilo 100 na kreti saba za soda iliyokuwa ikicheza na  bodaboda  ambayo nayo ilipata Sh 300,000 ngo’mbe mmoja, mchele kilo 100 na kreti ya soda.

Habari Zifananazo

Back to top button