DC Mwenda aongoza kikao tathmini ya lishe Iramba

Mkuu wa Wilaya ya Iramba mkoani Singida Suleiman Mwenda ameongoza kikao cha tathmini ya mkataba wa lishe jiongeze na tuwavushe salama kilichofanyika Januari 22,2024 kwenye ukumbi wa mikutano wa halmashauri.
DC Mwenda amepongeza mafanikio katika usimamizi na utekelezaji wa suala ya lishe wilayani Iramba hasa utoaji wa chakula shuleni ambapo jumla ya shule 140 sawa na asilimia 100 zimefanikiwa kutoa chakula kwa wanafunzi angalau mlo momja kwa siku, na jumla ya wanafunzi 76107 (99.57%) kati ya 77211 wanapata chakula cha mchana muda wawapo shuleni.

Aidha, DC Mwenda ametoa wito kwa watumishi wa Idara ya Afya kuendelea kuwahudumia kwa upendo akina mama wajawazito na kutoa elimu ya lishe kwa Jamii inayowazinguka
“Kubwa lingine ambalo tumeendelea kuhamasishana na bado halijafanyika kwa kiwango likubwa ni kuhusu kuwa na bustani za mboga mboga kwenye shule zetu, bado shule nyingi kwenye suala la bustani za mboga mboga limekwama. Kwa pamoja tunahitaji kuongeza juhudi ili kuhakikisha kwamba shule zetu hizi zinazalisha mboga kwaajili ya watoto kutumia pale shuleni,” amesema DC Mwenda.

Aidha Ofisa Lishe Wilaya ya Iramba, Naomy Sillah Amesema kuwa kwa kipindi cha robo ya pili mama wajawazito 11979 (99.6%) kati ya 12027 walihudhiria kliniki ya uzazi na mtoto, kupewa vidonge vya kuongeza damu vya madini chuma na asidi ya Foliki



