EU kuendelea kuiwekea vikwazo Urusi

UBELGIJI : MAWAZIRI wa Mambo ya Nje wa Umoja wa Ulaya wanakutana mjini Brussels, Ubelgiji, kujadili iwapo vikwazo dhidi ya Urusi vitapanuliwa kufuatia uvamizi wake nchini Ukraine.
Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya, Kaja Kallas, amesema anatarajia uamuzi wa kuendelea na vikwazo hivyo utapatikana, licha ya maoni ya Hungary, ambayo mapema mwezi huu ilisema bado haijafanya uamuzi wa kutoa msaada wake kwa mpango huo.
Uamuzi kama huu unahitaji kuungwa mkono na wanachama wote wa Umoja wa Ulaya kabla ya kuidhinishwa rasmi.SOMA: BELARUS: Lukashenko kuongoza muhula wa saba
Duru za kidiplomasia kutoka Ulaya zimeeleza kuwa makubaliano yamefikiwa na Waziri Mkuu wa Hungary, Viktor Orban, ambayo yataifanya nchi hiyo kuunga mkono mpango huo.
Kabla ya kuanza kwa mkutano huo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa, Jean-Noel Barrot, alithibitisha kuwa vikwazo dhidi ya Urusi vitaendelezwa.



