TFS yawakumbuka wazee kijiji cha Nunge

WAZEE wanaoishi kijiji cha Nunge kilichopo Wilaya ya Kigamboni, mkoani Dar es Salaam wamepatiwa msaada wa vitu mbalimbali ikiwa ni juhudi za Chama cha Tiger Friendship Society (TFS) katika kuiunga mkono serikali kuwajali wazee, kiafya, makazi na huduma zingine za jamii.

Septemba 29, 2019 akiwa mkoani Iringa, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alizindua kambi ya utoaji wa huduma za afya kwa wazee na watu wenye ulemavu katika viwanja vya Kichangani mjini Iringa ambapo aliitaka jamii kuwajali wazee ikiwamo kuwahudumia.

Akizungumza na wanahabari, Mwenyekiti wa Chama hicho, Kanali Mstaafu Elia Masangya amesema: “Kama chama cha wazee wastaafu, wameguswa kusaidia wazee wenzao wanaoishi katika makazi hayo kwa kuwapatia vitu mbalimbali vikiwemo na vyakula, nguo na mbao kwa ajili ya kukarabati paa la ukumbi wa mikutano vyote vikiwa na jumla ya zaidi ya Sh milioni 2.

Amesema chama hicho kilikubaliana  kutoa msaada huo kwa wazee wenzao waishio katika makazi yao ikiwa wakisheherekea kwa kutimiza miaka 25 tangu kuanzishwa kwake mwaka 2000 Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.

TFS ilianzishwa kwa lengo la kuwasiadia wazee wastaafu na watu wote wenye mahitaji muhimu, kubuni,kuanzisha na kuendeleza shughuli mbalimbali za kijamii, kiuchumi na mazingira yanayo wazunguka.

Naye Ofisa Ustawi wa Jamii Mwandamizi katika Makazi ya wazee hao, Jacklina Kanyamwenge ameushukuru uongozi wa chama hicho kwa msaada walioutoa kwani umesaidia kupunguza kwa kiasi fulani katika kutatua changamoto zinazo igusa makazi hayo.

Kwa kuna jumla ya vituo 13 nchini vinayo wahudumia watu wenye mahitaji mbalimbali vinavyo simamiwa na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum tunategemea ruzuku kutoka serikalini katika kuvihudumia vituo hivyo na hakuna vyanzo vyovyote vya kutuingizia fedha za kuviendesha vituo hivyo.

Bado tuna uhitaji wa chakula na vitu mbalimbali kwa makazi hayo, tunatoa wito kwa taasisi za serikali na binafsi kusaidia makazi hayo kwani bado kuna uhitaji katika kuwahudumia wazee na watu wenye uhutaji katika vituo mbalimbali nchini.

Kwa niamba ya wazee wa makazi hayo, Mussa Muna aliishukuru kwa msaada huo walioupokea na kuwaomba isiwe mwisho wa kutoa msaada katika kijiji chao kwani mahitaji bado ni mengi na huwa tunafarijika sana tunapo kumbukwa kwa hata hiko kidogo.

Tunaomba Asasi mbalimbali za kiraia na kidini kuendelea kutukumbuka katika misaada yao ya hali na mali nasi tufurahie maisha katika kipindi hiki cha kuishi katka makazi haya ya wazee na watu wenye mahitaji maalum.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button