Tshisekedi : Vijana jiungeni na jeshi kupambana na M23

CONGO : RAIS wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Felix Tshisekedi, amewataka vijana wa taifa hilo kujiunga kwa wingi na jeshi la taifa ili kusaidia kupambana na waasi wa M23 wanaojaribu kuchukua udhibiti wa maeneo makubwa zaidi mashariki mwa nchi.

Katika hotuba aliyoitoa kwa taifa, ambayo ilirushwa kwa njia ya televisheni, Tshisekedi aliwahimiza vijana kuchukua jukumu la kulinda nchi, akisisitiza kuwa wao ndiyo wanaowajibika kwa usalama na ulinzi wa Congo.

Vilevile, Rais Tshisekedi alikazia kwamba serikali yake inajiandaa kuwakabiliana na waasi hao kwa nguvu kubwa na kwa mbinu za kisasa, akiongeza kwamba M23 inapata msaada kutoka kwa Rwanda.

Alisema kwamba serikali ya Congo inajitayarisha kuanzisha kampeni yenye ustadi wa hali ya juu na mpango wa haraka dhidi ya waasi hao na washirika wao wa Rwanda.

Jumatano usiku, wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki walifanya mkutano wa mtandao na kutoa wito kwa Congo kuingia kwenye mazungumzo na makundi ya waasi, ikiwemo M23.

Hata hivyo, mkutano huo ulisusiwa na Rais Tshisekedi. SOMA: CONGO : Rais Tshisekedi asisitiza mapigano dhidi ya M23

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button