Kundi la M23 lajipanga kuuteka mji mkuu Kinshasa

CONGO : KUNDI la waasi la M23, linalotenda shughuli zake mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, limesema kwamba litaendelea kubaki katika mji wa Goma, ambao limeuteka, na pia linakusudia kuendelea mbele hadi mji mkuu, Kinshasa.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa waandishi wa habari waliokuwepo kwenye mkutano ulioitishwa na uongozi wa waasi wa M23 mjini Goma tarehe 30 Januari, kundi hilo limesema kuwa kutwaa kwao mji wa Goma haikuwa kazi rahisi.

Waasi hao, wanaoungwa mkono na Rwanda, wamesema lengo lao sasa sio tu kudhibiti Goma, bali pia kufika kwenye makao makuu ya nchi, Kinshasa. SOMA: Tshisekedi : Vijana jiungeni na jeshi kupambana na M23

Akizungumza na waandishi wa habari, mkuu wa muungano wa makundi ya silaha unaohusisha kundi la M23, Corneille Nangaa, alisema: “Tutaendelea na maandamano ya ukombozi moja kwa moja hadi Kinshasa.”

Wachambuzi wanasema kauli hii inaweza kumaanisha kuwa waasi hao wana dhamira ya kuiondosha serikali madarakani, jambo ambalo linaongeza mgogoro huo kwa kiwango kikubwa.

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button