Arumeru watakiwa kueleza mazuri ya CCM

VIONGOZI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya Arumeru mkoani Arusha wamehimizwa kueleza mazuri yanayofanywa na chama hicho na kuonesha jinsi chama kinavyofanya kazi katika kuwaletea maendeleo wananchi.
Mlezi wa CCM Mkoa wa Arusha ambaye ni mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Tanga Rajabu Abdulraham ametoa wito huo wakati maadhimisho ya miaka 48 ya kuzaliwa kwa CCM Wilaya ya kichama ya Meru.

Amesema ni vema pia wanachama wa chama hicho wakajua historia ya chama hicho ili kudumisha zaidi uimarisha wa CCM.

“Hao wanaopiga kelele watambue CCM imetoka mbali na ina historia yake hadi hapa tunaposherekea miaka 48 ya kuzaliwa kwake lakini waacheni watukejeli ila mwisho wa siku wananchi wataamua mbivu na mbichi kwenye sanduku la kura,”amesema.


