Benki Kuu ya Uganda yapoteza Bilioni 62

UGANDA: POLISI nchini Uganda imethibitisha kuwashikilia maafisa tisa wa Wizara ya Fedha kwa uchunguzi wa tuhuma za kudukua mifumo ya benki kuu na kuiba kiasi cha shilingi bilioni 62 (dola milioni 16.87).

Hii ni baada ya wizi mkubwa kutokea Novemba mwaka jana, ambapo Waziri wa Fedha, Henry Musasizi, alithibitisha kuwa akaunti za Benki ya Uganda zilidukuliwa na fedha kuhamishwa kinyume cha sheria.

Polisi imesema kuwa maafisa hao, wakiwemo kutoka idara ya hazina na ofisi ya mhasibu mkuu wa wizara, wanashikiliwa kwa ajili ya kusaidia uchunguzi wa tukio hilo.

Katika taarifa iliyotolewa, Wizara ya Fedha haikutaja majina wala idadi kamili ya maafisa waliokamatwa, lakini msemaji wa polisi, Kituuma Rusoke, alithibitisha kuwa maafisa hao wameshikiliwa na vyombo vya sheria.

SOMA Tanzania yang’ara sekta ya fedha Afrika

Gazeti la serikali la New Vision liliripoti kuwa wadukuzi hao, wakijitambulisha kama “Taka”, walifanikiwa kudukua mifumo ya TEHAMA ya Benki ya Uganda na kuhamisha fedha hizo kwa njia haramu.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button