Kabudi awaonya watangazaji kuacha kubananga Kiswahili

WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Palamagamba Kabudi amewaonya watangazaji wa  vyombo vya habari kuacha kubananga au kupotosha umma kuhusu matumizi sahihi ya lugha Kiswahili.

Akizungumza jijini Dodoma Leo kwenye Mkutano wa mwaka wa vyombo vya utangazaji nchini uliondaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Professa Kabudi amesema baadhi ya watangazaji wamekuwa wakipotosha umma kwa kutamka matamshi yasiyo sahihi akitolea mfano apa badala ya hapa, uyu badala ya huyu na wengi huwafuata.

“Tanzania tumefubaza Kiswahili kwa kudumaza kwa maneno kadhaa, kubananga Kiswahili matokeo yake watumiaji wengine wa nchi zinazotuzunguka wanaona hatuzungumzi kwa ufasaha.

“Watangazaji mna jukumu la kuhakikisha mnatangaza kwa lugha fanisi na fasaha. Vyombo vya Habari mna mchango mkubwa wa kusahihisha makosa mkiendelea hivyo, hilo ni janga litaigharimu nchi na kuacha kuwa kinara,”amesema.

Amezitaka mamlaka zinahusika kuwachukulia hatua watangazaji ambao hawazingatii maadili ya matamshi ya Lugha fasaha ya Kiswahili.

Pia, amewahimiza wamiliki wa vyombo vya habari kuweka vipindi vya kuelimisha kwa wingi kuliko kuweka burudani kwa muda mwingi na kuwachukulia hatua watangazaji ambao hawatumii matamshi kwa usahihi.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button