Walimu wa masomo ya Sayansi, Hisabati wapigwa msasa

HATUA madhubuti imechukuliwa ya kukabiliana na uhaba wa wataalamu wa sayansi kwa kuanzisha mafunzo endelevu kwa walimu wa masomo ya Sayansi na Hisabati.
Kwa mujibu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia mafunzo hayo yanatarajiwa kutatua changamoto ya uhaba wa wataalamu wa sayansi, kwa kuwa walimu watakaopata mafunzo watatumia mbinu walizojifunza kuwahamasisha na kuwafundisha wanafunzi kwa ufanisi zaidi.
Jumla ya walimu 1,071 kutoka mikoa ya Pwani, Dar es Salaam, na Morogoro wanashiriki mafunzo hayo yanayotolewa na Serikali kupitia Mradi wa Kuboresha Elimu ya Shule za Sekondari (SEQUIP).

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button