barawa atoa maagizo ATCL kukuza biashara

WAZIRI wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa ameliagiza Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) lihakikishe safari za ndege za shirika hilo zinafanyika kwa ratiba inayoeleweka.
Profesa Mbarawa alisema hayo Iringa jana wakati wa uzinduzi wa safari za ndege la shirika hilo kutoka Dar es Salaam kwenda Iringa baada ya miaka minane tangu kusitisha safari hizo.
Profesa Mbarawa amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa ATCL, Peter Ulanga aangalie idadi ya abiria wanaosafiri kutoka Iringa kwenda Dar es Salaam na kutoka Dar es Salaam kurudi Iringa katika ruti zake na kama abiria wataongezeka zaidi waongeze ruti zaidi kwa wiki.
Alisema katika uzinduzi huo ndege ilijaa kwa asilimia 100 tofauti na kwenye uzinduzi wa safari za ndege katika mikoa mingine.
Aidha, Profesa Mbarawa alishauri uwanja ukikamilika kwa asilimia 100 katika uwekaji wa taa wafikirie pia kuwa na safari za usiku kwenda na kutoka Dodoma, Dar es Salaam na maeneo mengine.
Alisema ATCL inahitaji kuongeza kiwango cha biashara kwa kuzingatia ubora wa huduma na akaagiza wasimamie kwa weledi na ubunifu ili kudumu katika soko la usafarishaji wa anga. Profesa Mbarawa aliliagiza shirika hilo lishughulikie malalamiko ya wateja haraka kuendana na soko na kutoa ushauri kuhakikisha linaweka bei inayolingana na huduma zinazotolewa na ndege.
Alimshukuru, Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha Kiwanja cha Ndege Nduli kimekami lika kwa asilimia 95 kwa kutoa zaidi ya Sh bilioni saba kukikarabati. Ulanga alisema ATCL itafanya safari tatu kwa wiki kwa nauli ya Sh 199,200 kwenda na kurudi ikijumuisha usafirishaji wa mzigo wenye uzito wa hadi kilo 23 na begi la mkononi lisilozidi kilo saba, bila malipo ya ziada.
“ATCL itaanza na safari tatu kwa wiki, kila Ju matatu, Jumatano na Ijumaa ambapo wanachama wa Twiga wataweza kulipia tiketi kwa kutumia pointi zao za safari,” alisema. Ulanga alisema kurejeshwa safari hizo kuta ongeza idadi ya watalii wanaotembelea mkoani Iringa sanjari na kurahisisha safari za wafanyabi ashara na wananchi wengine.



