Godfrey afariki safarini

MOROGORO: GODFREY Mbaga anayekadiliwa kuwa umri wa miaka 25-30 ambaye ni mkulima na mkazi wa Mwanza, amefariki dunia wakati akiwa safarini akitoka Mwanza kuelekea Dar es Salaam baada ya kuanza kujisikia vibaya.

Taarifa hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi mkoani Morogoro SACP Alex Mkama, ambapo amesema tukio hilo limetokea Februari 23, 2025 majira ya asubuhi katika eneo la Mikese wilayani Morogoro.

Amesema Godfrey alianza kujisikia vibaya na alifikishwa katika hospitali ya Rufaa mkoani Morogoro kwa ajili ya kupatiwa matibabu lakini hakupata nafuu na hatimaye alifariki dunia, na maiti yake imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali hiyo kwa ajili ya utambuzi na uchunguzi.

Godfrey amekutwa na mkasa huo akiwa katika basi la kampuni ya Ally’s lenye namba za usajili T 433 EBG lililokuwa likiendeshwa na Emanuel Kayanda.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button