Rihanna kuja na albamu ya tisa

BAADA ya kusubiri miaka mingi na mashabiki kusubiri kwa hamu, hatimaye Msanii kutoka Marekani, Robyn Fenty ‘Rihanna ameithibitisha ujio wa albamu yake ya tisa.

Rihanna amethibitisha katika mahojiano na Harper’s Bazaar.

Mrembo huyo mwenye umri wa miaka 37, alijulikana zaidi kwa hiti lake la kwanza, “Pon de Replay,” akiwa na miaka 17. Ingawa alitoa albamu yake ya “Anti” mwaka 2016, tangu wakati huo alijikita zaidi katika biashara kama Fenty Beauty na Savage x Fenty. Hata hivyo, mashabiki wake wamekuwa wakisubiri kwa hamu albamu yake ya tisa (R9).

Katika mahojiano hayo, Rihanna alisema kwamba alikuwa akitafuta mwelekeo sahihi kwa kazi yake mpya. Alisema kuwa alisikiliza tena albamu yake ya “Anti” ili kujua ni wapi anataka kuelekea na albamu hii ya tisa.

Hata hivyo, alisisitiza kuwa hakutaka kutoa muziki usiolingana na ukuaji wake wa kisanii. “Siwezi kutoa kitu cha kawaida,” alisisitiza Rihanna.

Pamoja na uvumi kwamba albamu yake mpya ingekuwa na ladha ya reggae, Rihanna alikanusha na kusema kuwa hana mipaka yoyote ya aina ya muziki kwa sasa.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button