Wanahabari tumieni teknolojia ya akili mnemba-AI

DAR-ES-SALAAM : MKURUGENZI wa Shirika la TMC linaloshughulikia maendeleo ya Tehama nchini, Asha Abinallah, amewashauri wadau wa vyombo vya habari kubadilisha mitazamo ya kufanya kazi kwa njia za kizamani na kuanza kutumia teknolojia ya akili mnemba (AI).

Akichambua matokeo ya utafiti kuhusu matumizi ya teknolojia ya akili mnemba  (AI) kwa maendeleo ya vyombo vya habari, Asha amesema kuwa maendeleo ya teknolojia ya AI yanaenda kwa kasi kubwa, na hivyo wadau wa habari hawana budi kubadilika ili kwenda sambamba na mabadiliko ya teknolojia.

“Hatuwezi kusema tutakwenda na mabadiliko bila kubadilisha mtindo wa kufanya kazi. Hatuwezi kudai kwamba tutatumia AI na kunufaika nayo bila kubadilisha mitazamo yetu na kukubali kwamba teknolojia ni muhimu. Ili kufanikisha hili, ni lazima tuiweke katika matumizi kwa faida yetu,” alisisitiza Asha.

Aidha, Asha alitoa wito kwa wadau hao kuendelea kushirikiana na wenzao kutoka ndani na nje ya nchi ili kupata ujuzi zaidi kuhusu teknolojia ya akili  mnemba na kwenda sanjari na mabadiliko ya maendeleo ya Tehama nchini.

SOMA: “Teknolojia imeleta aina mpya ya ukatili”

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button