Silafrika yaipongeza serikali sera rafiki uwekezaji

KAMPUNI ya SILAFRIKA imeipongeza serikali kwa msaada na sera rafiki kwa wawekezaji kwani inachangia ukuaji wa pato la taifa.

Kauli hiyo imetolewa hivi karibuni katika maadhimisho ya miaka 35 ya kampuni hiyo yaliyofanyika katika Dar es salaam na Mkurungenzi Mtendaji wa SILAFRIKA, Alpesh Patel.

“Sera zinatuunga mkono sana, na hiyo imekuwa sehemu muhimu ya mafanikio yetu na ndio maana leo tumekutana na mawakala zaidi ya 60 kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania ilikurudisha shukrani kwao kutokana na kile wanachokifanya ikiwa ni maadhimisho ya miaka 35 tangu kuanzishwa kwa kampuni yetu,”amesema.

Mkurugenzi Mtendaji wa SILAFRICA nchini, Alpesh Patel, amesema kampuni hiyo inaendelea kujikita katika kutoa bidhaa za kuaminika na za hali ya juu, huku mahitaji ya uhifadhi wa maji yakiendelea kuongezeka.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button