Papa Francis ashindwa kuendesha ibada ya majivu

VATICAN: KIONGOZI Mkuu wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis, ambaye bado amelazwa hospitalini kutokana na matatizo ya kupumua, anaendelea vizuri.
Taarifa zinasema kuwa licha ya Papa Francis kuendelea vizuri, ameshindwa kuongoza ibada muhimu ya Jumatano ya Majivu, inayofungua kipindi cha siku 40 za mfungo wa Kwaresma.
Kwa kawaida, Papa Francis mwenye umri wa miaka 88 huongoza ibada hiyo, lakini kwa leo misa hiyo itaongozwa na Kadinali wa Italia, Angelo de Donatis, na kutanguliwa na maandamano kwenye kilima cha Aventine huko Roma.
Kulingana na imani ya Kikristo, mfungo wa Kwaresma hufanyika siku 40 kabla ya sherehe ya Pasaka, ikikumbushia siku alizozitumia Yesu Kristo kufunga akiwa jangwani.
SOMA: Papa Francis, asumbuliwa homa ya mapafu



