Deby anyakua viti 43 kati 46 vya seneti

CHAD: CHAMA cha kiongozi wa kijeshi wa Chad, Mahamat Idriss Deby, cha Deby’s Patriotic Salvation Movement (MPS), kimeshinda viti 43 kati ya 46 katika uchaguzi wa kwanza wa seneti uliofanyika mwishoni mwa mwezi Februari.

Uchaguzi huo ulifanyika kama sehemu ya hatua ya mwisho ya mageuzi ya kisiasa yenye lengo la kuimarisha zaidi utawala, mageuzi ambayo yalianza baada ya Deby kuchukua mamlaka kufuatia kifo cha baba yake miaka minne iliyopita.

Deby alishinda muhula wa miaka mitano kama rais mwezi Mei mwaka jana katika uchaguzi ambao ulikosolewa na upinzani, huku mashirika ya kimataifa yasiyo ya kiserikali yakisema uchaguzi huo haukuwa wa huru na haki.

SOMA: PSM yaongeza viti vya wabunge Chad

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button