Makalla ataja mabadiliko sheria ya uchaguzi

KATIBU wa Halmashauri Kuu Taifa (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Amos Makalla amesema kuwa serikali imefanya mabadiliko katika sheria ya uchaguzi chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan baada ya kusikia malalamiko juu ya mabadiliko ya katiba hususani kutoka kwa vyama vya upinzani.

Makalla ambaye pia Mlezi wa Mkao wa Dar es salaam CCM ameeleza hayo leo Machi 5,2025 wakati akizungumza katika Mkutano wa Viongozi wa Chama na Jumuiya ngazi ya Shina, Tawi, Kata na Wilaya katika Wilaya ya Ubungo mkoani Dar es salaam, ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya siku tano katika mkoa huo.

Akifafanua mabadiliko hayo Makalla amesema Rais Samia aliposikia hoja hizi za kufanyika mabadiliko ya katiba hususani katika sheria ya uchaguzi kutoka kwa wadau mbalimbali aliunda kikosi kazi kwa ajili ya kukusanya maoni na kutoa ushauri juu ya sheria zilizopi na akamteua prof Rwekaza Mkandala kuwa mwenyekiti wa kikosi hicho ili kuweza kufanya mabadiliko.

Ameongeza kuwa kupitia kamati hiyo viliitwa vyama vyote vya siasa nchini kukutana na kutoa maoni na vyote vilishiriki isipokuwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwani walisema walitaka kusikilizwa wakiwa peke yao.

Makalla amesema kuwa walimfata aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM, Abdulrahman Kinana walikabidhi taarifa kwa Rais Samia na bila kusita uliandaliwa mswada wa sheria na kupelekwa bungeni.

Kamati ya bunge ilikaa na kukusanya maoni na ikapatikana sheria mbili ikiwemo sheria mpya ya Tume huru ya uchaguzi na kamati ya usaili itakayoongozwa na Jaji Mkuu wa Tanzania na Zanzibar na wajumbe fulani na katibu ya kamati ya tume ya mamlaka ambao watapeleka maoni ili rais aweze kuteuliwa.

Pia amesema kupitia mabadiliko hayo Rais hawezi kubadilisha wala kuteua wajumbe wapya wa tume hadi kamati kuu ikae na kufanya maamuzi kwa kupitia majina na kuyapelekwa ka rais ili awese kuamu.

“Ukisema mabadiliko ya katiba yanahusisha mambo mengi na wadau wengi lakini sio mabadiliko ya sheria ya uchaguzi kama wao wanavyokimbilia kusema,” amesema Makalla.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button