Niko tayari kurejesha amani Ukraine- Zelensky

UKRAINE : RAIS wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, amesema kuwa muafaka wa amani na Urusi unaweza kufikiwa endapo Urusi itakubaliana kurejesha amani.

Zelensky alisisitiza kuwa hana kinyongo baada ya mkutano uliokumbwa na mkanganyiko na Rais waarekani, Donald Trump, wiki iliyopita na kumshukuru Trump kwa uongozi wake na msaada wa silaha kwa Ukraine.

Kupitia mtandao wa X, Zelensky alisema kuwa Ukraine iko tayari kukaa kwenye meza ya mazungumzo haraka iwezekanavyo ili kuleta amani ya kudumu.

Huu ni msimamo wake kufuatia tuhuma kutoka Marekani kuwa Ukraine haiko tayari kumaliza vita vyao, jambo lililosababisha Trump kusimamisha msaada wa kijeshi kwa Kiev.

Zelensky alisema kuwa hatua za kwanza za amani huenda zikajumuisha kuachia wafungwa, kusitisha mashambulizi kutoka angani—ikiwemo makombora, droni za masafa marefu, na mashambulizi ya mabomu kwenye miundombinu ya nishati na miundombinu ya kiraia—pamoja na kusitisha mashambulizi ya baharini. Alisema hatua hizi zitatekelezwa ikiwa Urusi nayo itachukua hatua zinazolingana.

Aidha, Zelensky aliongeza kuwa anatumai kuanzisha upya uhusiano na Washington na kwamba bado yuko tayari kusaini makubaliano kuhusu usalama wa madini ili Marekani iweze kuhakikisha usalama wa Ukraine.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button