RC Mtwara azindua ugawaji misaada waathirika mafuriko

MKUU wa Mkoa wa Mtwara Kanali Patrick Sawala amezindua na kukabidhi rasmi zoezi la ugawaji wa msaada mbalimbali kwa waathirika wa mafuriko katika Manispaa ya Mtwara Mikindani mkoani Mtwara kufuatia mvua zilizonyesha Februari 2025.

Akizungumza leo wakati wa hafla fupi ya kuzindua na kukabidhi vifaa hivyo kwa waathirika hao, mkuu huyo wa mkoa ameishukuru serikali  na wadau mbalimbali wajitolea kuchangia msaada huo.

Msaada huo umetolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu pamoja na wadau mbalimbali ambapo miongoni mwa msaada huo uliyotolewa ikiwa ni pamoja na chakula, magodoro na vingine lengo ni kuwafuta machozi waathirika hao.

Sawala ametoa rai kwa wananchi wa manispaa hiyo na Mtwara kwa ujumla kuweka nyumba zao katika hali ya uimara ili kuzuia madhara hayo yasijitokeze tena.

Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mwaipaya amesema mbali na kuwashukuru wadau waliojitolea misaada hiyo, amewashukuru wananchi waliojitoa na kuwapatia hifadhi wananchi wenzao waliopatwa na atha hiyo na kuwataka watendaji kusimamia kikamilifu zoezi hilo la ugawaji kwa wahusika.

Aidha, mafuriko hayo yamesababishwa na mvua kubwa zilizonyesha kuanzia Februari 3 hadi 7 mwaka huu ambapo ni takribani mwezi mmoja mpaka sasa na kuleta athari kwa waathirika takribani 900 kwa madhara tofauti tofauti ikiwemo kubomolewa nyumba, kuharibu miundombinu mbalimbali na mengine.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button