Utafiti changamoto za elimu jumuishi waanza

WIZARA ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na mpango wa shule bora wanatarajia kuendesha utafiti wa pamoja wenye lengo la kuimarisha usalama na ujumuishi wa wanafunzi katika shule za msingi nchini.

Akizungumza katika uzinduzi wa utafiti huo katika hafla ya uzinduzi iliyofanyika kwenye viwanja vya Kigano Halmashauri ya Mji wa Kasulu mkoani Kigoma, Mratibu wa Mpango wa Shule Bora, Morris Mkotya amesema kuwa huo utafanyika kwenye mikoa minne ambapo kila mkoa utatoa halmashauri moja.

Kamishna wa elimu nchini, Dk Lwabene Mtahaba ambaye amemwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Carolyne Nombo akizundua utafiti wa usalama na elimu jumuishi nchini.

Morris amesema kuwa utafiti huo unakuja baada ya kuanza kutekelezwa kwa mpango wa shule bora na kugundua kukosekana kwa mfanano katika utekelezaji wa taratibu za usalama shuleni, kiwango kisichoridhisha cha utekelezaji wa elimu jumuishi Sambamba na ushiriki mdogo wa jamii katika kusaidia watoto mwenye mahitaji maalum.

Akizindua utafiti huo Kamishna wa Elmu nchini, Dk Lwabene Mtahaba ambaye amemwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Profesa Carolyne Nombo amesema Tanzania imepiga hatua kubwa katika masuala ya elimu ikiweka msisitizo katika elimu jumuishi na usalama wa watoto bila ubaguzi.

Ofisa Elimu wa Mkoa Kigoma Pauline Ndigeze

Dk Lwabene amesema matokeo ya utafiti huu yatasaidia kufanya maboresho kwenye sera na sheria za elimu ambazo zitasaidia kuimarisha mfumo wa elimu nchini ili kuhakikisha kuwa kila mtoto anapataa fursa sawa ya kujifunza na kufikia ndoto zake.

Akizungumza katika uzinduzi huo Afisa elimu katika sekretariet ya Mkoa Kigoma, Paulina Ndigeze amesema wamepokea fursa ya kuwa moja ya mikoa ambayo utafiti huo utafanyika na wanaamini kuwa matokeo ya utafiti huo yatakuwa na chachu kubwa katika kuhakikisha usalama na elimu ya jumuishi kwa wanafunzi wote.

Baadhi ya wanafunzi wa shule za msingi wilayani Kasulu waliohudhuria uzinduzi huo

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button