TCRA yaanza kuziba pengo la wasichana kwenye TEHAMA

DAR ES SALAAM: amlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeanza kwa kishindo maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wasichana katika TEHAMA 2025 kupitia programu ya mafunzo ya siku tano iliyotolewa kwa wanafunzi wa kike wenye mahitaji maalum kutoka Shule za Sekondari Jangwani na Mbweni Teta  katika Shule ya Sekondari Kijitonyama Sayansi, Dar es Salaam.

Akielezea programu hiyo iliyoanza kuanzia tarehe 10-14 Machi 2025, Mhandisi Mwanahamisi Suleiman ambaye pia ni mwanakamati ya maandalizi ya maadhimisho haya kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) amesema, “Wanafunzi hao wameendelea kujifunza kwa vitendo kwa kutoa mawazo, kuwasilisha, na kisha kubuni mifumo inayotatua changamoto kulingana mahitaji ya mtumiaji husika (user-centric design) katika jamii yao.”

TCRA mwaka huu imejipanga kufikia makundi tano ya wanafunzi wa kike kuelekea maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wasichana katika TEHAMA 2025 tarehe 24 Aprili 2025.

Makundi hayo ni pamoja na wasichana wa kike kutoka shule za awali, msingi, Sekondari na wenye mahitaji maalumu kutoka sekondari na wanavyuo.

SOMA: Mambo yaiva tamasha la kuombea Uchaguzi Mkuu

Ni miaka saba sasa tangu maadhimisho hayo yalipoanzishwa rasmi kupitia shirika la Mawasiliano Duniani (ITU) na TCRA kama mwanachama imewafikia wasichana zaidi ya elfu nne (4,000) kwa lengo la kuwahamasisha na kuwatia moyo wasichana na wanawake vijana wanaosoma masomo Sayansi, Teknolojia, Uhandisi, na Hisabati (STEM), na kujihusisha ya shughuli za sekta ya TEHAMA, ili kupunguza pengo la kijinsia katika tasnia hii na hivyo kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) hasa lengo namba 5.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button