DAR ES SALAAM; Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Kuombea Uchaguzi mkuu 2025, Alex Msama amesema maandalizi kuhusu tamasha hilo yanaenda vizuri.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, amesema tamasha hilo la waimbaji wa nyimbo za Injili litafanyika Aprili 20, 2025 jijini Dar es Salaam na baadaye litaenda mikoa mingine 26.
“Maandalizi ya tamasha yanaendelea vizuri na tunakaribisha wadhamini kuja kusaidia kufanikisha tamasha hili kubwa ambalo litafanyika mikoa yote ya nchi yetu ya Tanzania tukianzia na Mkoa wa Dar es Salaam,” amesema na kuongeza:
“Kwa sasa jambo kubwa linalofanyika ni kuendelea kuzungumza na wafadhili na tukifanikiwa tu kupata wadhamini basi tamasha litakuwa halina kingilio litakuwa bure.”
Tamasha la kuombea uchaguzi litahusisha waimbaji mbalimbali wa nyimbo za Injili ndani na nje ya Tanzania.
I was BROKE and desperate… now I make $3,000+ weekly from my couch! Just 30 days ago, I was stuck in a dead-end job, living paycheck to paycheck. Then I found this secret method—and everything changed Anyone can do this in their free time. Spots are LIMITED! Don’t miss out!
Join now➤➤ http://Www.WorksProfit7.Com