Waandishi wa habari kusajiliwa kidigitali

PWANI: SERIKALI itazindua mfumo mpya utakaowaandikisha waandishi wa habari kwa njia ya kidijitali ambapo mfumo huo utaboresha usajili wao sambamba na kuendana na mabadiliko ya kiteknolojia katika sekta ya habari.

Msigwa ametoa taarifa hiyo leo Machi 16, 2025 akiwa katika Bandari Kavu ya Kwala, mkoani Pwani ambapo amesema uzinduzi wa mfumo huo utafanyika mwisho wa mwezi huu.

“Mwisho wa mwezi huu tutazindua mfumo utakao ratibu usajili wa waandishi wa habari. Kufika mwezi wa 4, mwandishi wa habari wa Tanzania hatatembea na kitabu, atakuwa na kadi ya kidijitali. Ukienda sehemu, unamwambia, ‘Mimi ni Mwandishi wa habari,’ kadi yako ina QR code inayo taarifa za siri ndani yake. Ukimuonesha, akipiga hiyo QR code, itampeleka kwenye tovuti ya Serikali, itamuonesha taarifa zako,” amesema Msigwa.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button