Vifaa vya ujenzi vinajitosheleza nchini-Serikali

SERIKALI imesema vifaa vya ujenzi vinavyozalishwa hapa nchini vinajitosheleza na hakuna faida ya watanzania kuendelea kununua kutoka nje ya nchini.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Prof. Kitila Mkumbo amesema hayo Mjini Kibaha katika ziara ya siku moja kukagua uzalishaji unaofanyika katika kiwanda cha Kinglion kinachounganisha pikipiki na kutengeneza mabati

Waziri Mkumbo amesema kwa sasa hakuna haja ya kununua vifaa vya ujenzi kutoka nje ya nchi kutokana na kuwepo kwa viwanda vingi vinavyotengeneza vifaa hivyo ikiwemo London, saruji na mabati.

“Kwa sasa nchi yetu inajitosheleza katika vifaaa vya ujenzi na hakuna sababu yeyote ya mtanzania kuagiza vifaa hivyo nje maana kwanza ni gharama kubwa sana hivyo niendelee kuwahimiza watanzania kununua bidhaa hizo hapa nchini”alisema

“Serikali imebodesha mazingira ya uwekezaji na tunaendelea kutenga bajeti kwa ajili ya kutatua changamoto za miundombinu ya barabara katika maeneo ya uchuni hususani viwandani” amesema.

Aidha alisema kiwanda hicho ambacho ni kati ya viwanda vikubwa Afrika kimekuwa kikiuza biashara zake ndani na nje ya nchi na kwamba kutokana na vifaa vyake wanaongezeka nchi uwezo wa kushindana kwenye masoko ya kimataifa.

“Hapa wana maabara zao kabla ya Shirika la viwango kuja kuzikagua na wamekuwa wakiuza nje ya nchi wanatutangaza huko duniani tutawapa ushirikiano kutatua vikwazo walivyonavyo kuwaondolea ukwamo wa biashara,” alisema.

Amepongeza Uwekezaji wa kiwanda cha Kinglion ambacho tayari kwasasa wametumia milioni 42 kuwekeza sambamba na kutoa ajira 2000 kati ya hizo 800 za moja kwa moja na 1200 za muda.

Kadhalia alisema Serikali inaendelea kusimamia kwenye uwekezaji wa viwanda hivyo viweze kulipa wafanyakazi kwa kuzingatia viwango vinavyotakiwa.

Meneja wa kiwanda hicho, Anold Lyimo aliishukuru Serikali kwa ushirikiano wanaowapatia katika shughuli zao za Uwekezaji huku akisema vikwazo wanayokabiliana navyo tayari wameviwasilisha kuomba vitatuliwe.

Lyimo amebainisha mambo ambayo yanahitaji kufanyiwa kazi na serikali kuwa ni pamoja na kuunganishiwa nishati ya gesi na kuboreshewa barabara inayoingia kiwandani.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button