CCM kifua mbele uchaguzi mkuu

MBEYA: CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kinakwenda katika uchaguzi wakiwa wanajivunia rekodi ya maendeleo yaliyofanyika chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.

Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Amos
Makalla ameyasema hayo leo Machi 27,2025 wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Ruanda Nzovwe Wilaya ya Mbeya ya Mjini mkoani Mbeya ikiwa ni mwanzo wa ziara yake ya siku tatu mfululizo katika mikoa miwili ya Mbeya na Iringa.

Aidha, Makalla amesema anahistoria na Mkoa wa Mbeya kwani alishawahi kuwa Mkuu wa Mkoa huo kuanzia Machi 16,2026 hadi Agosti 2018 aliposhamishiwa katika Mkoa wa katavi katika uwanja wa ndege uliopo Songwe mkoanj Mbeya hakukuwa na taa lakini katika uongozi wa Rais Samia alitoa Sh bilioni 4 kwa ajili ya kutengeneza.

Ameongeza kuwa katika uwanja huo yamefanyika maboresho katika jengo la abiria kwa kutumia kiasi cha Sh bilioni 12 ambazo zimetolewa katika uongozi wa Rais Samia.

Akifafanua maendeleo hayo Makalla amesema suala la barabara nne kwa mkoa wa Mbeya ilikuwa ni historia na lilikuwa likiongelewa kila kukicha lakini serikali chini ya Rais Samia imetolewa Sh bilion 138 kwa ajili ya utekelezaji wa ujenzi wa barabara ya njiane katika mkoa huo.

Pia ameeleza kuwa kinachokwamisha kuendelea kwa utekelezaji wa mradi huo na kusimama ni kutokana na amvua zinazoendelea lakini mkandarasi ameshalipwa Sh bilioni 15.6 kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa mradi huo wa barabara.

“Changamoto iliyopo hapo sio fedha mkandarasi amelipwa fedha zaidi ya Sh bilioni 15.6 kinachokwamisha ni mvua mvua hizi lakini tumeagiza serikali na mkua wa mkoa wapo wanasimamia kwahiyo ujenzi utaendelea kwa kasi,” amesema Makalla.

Aidha, Makalla amesema wanaendelea na utekelezaji wa ujenzi wa barabara wa zaidi ya Kilometa 23 kwa zaidi ya Sh bilioni 28 zinatumika katika ujenzi wa barabara hiyo pia amesema katika mkoa huo kumekuwa na changamoto ya maji lakini upo unatekelezwa mradi wa maji.

Makalla amesema katika mradi huo na hadi sasa mkandarasi ameshalipwa bilioni 21 na mradi huo umedikia asilikia 40 ya utekelezaji wake na kukamilika kwake itakuwa ni mwisho wa tatizo la maji katika mkoa wa Mbeya.

Pia mabadiliko mengine ni katika kilimo kwa kuongezeka kwa bei na thamani ya kuuza mazao hususani katika mazao ya biashara yakiwemi mazao ya Pareto, Tumbaku na Kokoa ambayo imetoka kuuzwa 2800 hadi kufikia 25,531 na yote hayo ni sehemu ya maendeleo yaliyotokana na jitihada za serikali ya awamu ya sita.

Makalla amesisitiza kuwa kutokana na maendeleo na mabadiliko lukuki wanaimani itakuwa ni nguzo na ushindi katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Mwaka huu.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button