Kagame aikosoa Jumuiya ya Kimataifa

KIGALI: RAIS wa Rwanda, Paul Kagame, amezikosoa nchi zinazoiwekea Rwanda vikwazo kufuatia mzozo unaoendelea mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).
Akiwa kwenye hafla ya kuadhimisha kumbukumbu ya mauaji ya kimbari ya mwaka 1994, Kagame alisisitiza kuwa nchi hizo zinapaswa kutatua matatizo yao wenyewe badala ya kuingilia masuala ya Rwanda.
Hali bado nchini DRC imekuwa mbaya, ambapo waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda wamechukua baadhi ya maeneo, ikiwa ni pamoja na miji ya Goma na Bukavu.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa wataalamu wa Umoja wa Mataifa wamedai kuwa Rwanda inaaskari 4,000 nchini DRC wakisaidia waasi hao.
SOMA: Majaliwa akutana na mabalozi wa Tanzania nchi za Zimbabwe, Rwanda
Kufuatia hali hii, Umoja wa Ulaya umeweka vikwazo dhidi ya makamanda watatu wa Rwanda, huku Marekani ikimfungia waziri mmoja wa serikali.
Aidha, Uingereza, Canada, na Ujerumani nazo zimetangaza kusitisha baadhi ya misaada na vibali vya biashara na Rwanda, hali inayoashiria mvutano unaoendelea kati ya Rwanda na jumuiya ya kimataifa.



