Mzee wa miaka 80 ashukuru kujengewa nyumba

“CHA kuwapeni mimi sina, Mungu atawalipa” maneno ya mzee Hamisi Seleman mkazi wa Mtwara Mjini, mkoani Mtwara baada ya kujengewa nyumba yenye hadhi na kutolewa kwenye nyumba chakavu aliyokuwa akiishi.
Mzee huyo mwenye umri wa miaka zaidi ya 80, alipata neema ya kujengewa nyumba na waumini wa KKKT Kanisa Kuu la Mtwara pamoja na watu mbalimbali kutoka nje na ndani ya nchi mwezi baada ya kutambuliwa akiwa anaishi kwenye kibanda chakavu na kuhatarisha maisha yake wakati wa mvua.
Askofu Msaidizi wa Kanisa hilo, Geoffrey Mposola ameiomba serikali kujenga kituo cha kulelea wazee wenye mahitaji.
Amesema kuwa wazee wengi wenye uhitaji wanatembezwa Mtwara kuomba msaada wengi wao wakiwa hawana watoto. Nyumba ya Mzee Hamisi Seleman imejengwa kwa thamani ya zaidi ya Sh milioni 5.



