Marekani, Ulaya, Ukraine kujadili mzozo wa Urusi

PARIS : VIONGOZI wa ngazi za juu wa Marekani, Umoja wa Ulaya na Ukraine wanatarajiwa kukutana Alhamisi mjini Paris kujadili hatma ya mzozo kati ya Urusi na Ukraine, pamoja na hali inayokwama katika juhudi za amani.

Mkutano huo utahudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Marco Rubio, Mjumbe wa Rais wa Marekani, Donald Trump, Steve Witkoff, Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron, pamoja na waziri wake wa mambo ya nje, Jean-Noel Barrot.

SOMA: Urusi yaipongeza Ukraine utayari kumaliza vita

Ukraine itawakilishwa na Waziri wa Mambo ya Nje, Andrii Sybiha, sambamba na mkuu wa ofisi ya Rais, Andriy Yermak. Yermak amesema kuwa watakutana pia kwa mazungumzo na viongozi wa Ujerumani na Uingereza kuhusu suala la dhamana ya usalama, ikiwa kutafikiwa mpango wa amani katika eneo hilo.

Mkutano huu unakuja katika kipindi ambacho juhudi za kimataifa za kutafuta amani zinas hamasishwa, huku mzozo huo ukiendelea kutishia usalama katika eneo la Ulaya na zaidi. Wadau hao wanatarajia kujadili njia za kuwezesha mazungumzo yenye tija na kuleta suluhu ya kudumu kwa mgogoro unaoendelea.

Habari Zifananazo

One Comment

  1. Single Mom Reveals How She Earns $89k/Yr Working 10 Hrs/Week From Home. Tired of paycheck-to-paycheck living? Meet Kelly from New York—a regular mom who cracked the code to recession-proof income without selling a thing! Now, YOU can too with the Home Profit System:

    ACT NOW➢ https://Www.earnapp1.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button