Prisons, KMC vitani kujinasua

DAR ES SALAAM – TANZANIA Prisons na KMC zinakabiliwa na mtihani wa kujinasua kwenye nafasi za chini kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara zitakapokabiliana na JKT Tanzania na Dodoma Jiji.
Prisons inayoshika nafasi ya 14, ikiwa na pointi 24 baada ya michezo 26 itaikaribisha JKT Tanzania inayoshika nafasi ya saba, ikiwa na pointi 32 ikicheza michezo 25 Uwanja wa Sokoine, Mbeya.
Nayo KMC iliyo nafasi ya 13, ikiwa na pointi 27 baada ya kucheza mechi 25 itakuwa mwenyeji wa Dodoma Jiji yenye pointi 34 baada ya kucheza michezo 26 katika Uwanja wa KMC Complex, Mwenge, Dar es Salaam.
Kama Prisons itashinda mchezo huo dhidi ya JKT itafikisha pointi 27 na kulingana na KMC lakini zitatofautiana kwa mabao ya kufunga na kufungwa.
Lakini kama JKT ikishinda itafikisha pointi 35 na kuishusha Dodoma Jiji yenye pointi 34 kwenye nafasi ya sita. Ushindi kwa Dodoma Jiji dhidi ya KMC utaifanya kufikisha pointi 37 na kulingana na Tabora United iliyo nafasi ya tano lakini zikitofautiana kwa mabao ya kufunga na kufungwa.
Hata hivyo, kama KMC itaifunga Dodoma Jiji itafikisha pointi 30 na kupanda mpaka nafasi ya tisa ikizishusha Pamba Jiji (27), Namungo (28), Coastal Union (28) na Fountain



