Che Malone awatoa hofu awatoa hofu mashabiki mashabiki Simba

DAR ES SALAAM – BEKI wa Simba, Che Fondoh Malone amewatoa hofu mashabiki wa timu hiyo kuelekea mchezo wao wa hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Stellenbosch, Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar Jumapili.

Akizungumza wakati wa mazoezi ya timu hiyo jana, Malone alisema kwa upande wao wanaamini kila kitu kitaenda sawa, hivyo wana matumaini ya kushinda mchezo huo.

“Ni imani yetu tutacheza vyema na kushinda hapa nyumbani, nitumie nafasi hii kuwakaribisha mashabiki watuunge mkono kwa sababu tunafahamu mchezo wa pili Afrika Kusini utakuwa mgumu, hivyo tukipata matokeo mazuri hapa Zanzibar tutafuzu fainali,” alisema Malone.

Beki huyo raia wa Cameroon aliyekosa mechi za robo fainali dhidi ya Al Masry, alirejea hivi karibuni kutoka Morocco alikokuwa akipatiwa matibabu baada ya kuumia kwenye mchezo dhidi ya Azam uliomalizika kwa sare ya mabao 2-2.

Simba wanawania kucheza fainali yao ya kwanza ya michuano hiyo baada ya mara ya mwisho kufanya hivyo mwaka 1993 walipolikosa kombe nyumbani kwa kufungwa mabao 2-0 na Stellah Abidjan

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button