Simba yatinga fainali Afrika

AFRIKA KUSINI; SIMBA imetinga fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, baada ya leo kutoka 0-0 mchezo wa marudiano nusu fainali dhidi ya wenyeji wao Stellenbosch FC ya Afrika Kusini Uwanja wa Moses Mabhida mjini Durban.

Kutokana na matokeo hayo Simba imesonga mbele kwa jumla ya bao 1-0 kutokana na ushindi iliyoupata mchezo wa kwanza baina ya timu hizo uliofanyika Jumapili iliyopita Uwanja wa Amaan mjini Zanzibar.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button