Amnesty yaikosoa serikali ya Trump

MAREKANI: SHIRIKA la Kimataifa la Kutetea Haki za Binadamu, Amnesty International, limetoa ripoti yake ya kila mwaka na kukosoa vikali hatua za Rais wa Marekani, Donald Trump, ambaye ametimiza siku 100 za muhula wake wa pili madarakani.
Katika ripoti hiyo, Amnesty imesema kuwa hatua za Trump zinahatarisha mafanikio ya kimataifa katika vita dhidi ya umaskini, mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi, na kulinda haki za binadamu.
Tangu aapishwe Januari 20, Trump amechukua hatua mbalimbali za kiuchumi, kijamii na kiusalama, ikiwa ni pamoja na kuongeza ushuru, kusitisha misaada ya kimataifa, kuzua sintofahamu na washirika wa NATO, pamoja na kutoa vitisho vya kutwaa maeneo kama Gaza, Greenland, Mfereji wa Panama, na hata kutaka kuifanya Canada kuwa jimbo la 51 la Marekani.
SOMA: Marekani: Vifaa vya simu,elekroniki vyapandishwa ushuru



