Marekani yaitetea Israel kuzuia misaada Gaza

UHOLANZI : MAREKANI imeitetea Israel mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ), kuhusu uamuzi wake wa kuzuia misaada ya kibinadamu kuingia Gaza, ikisema hatua hiyo inalenga kulinda usalama wake.

Wakili wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, Josh Simmons, amesema Israel ina maslahi halali ya kiusalama na kwamba misaada inapaswa kupelekwa kwa uangalizi mkubwa ili isije kutumiwa na makundi ya kigaidi.

Simmons amesema Marekani inaunga mkono upatikanaji wa misaada kwa raia wa Gaza, lakini akasisitiza kuwa kuna haja ya tahadhari kubwa katika ugawaji wake.

Kesi hiyo, iliyofunguliwa wiki hii katika makao ya ICJ mjini The Hague, inalenga kuangazia wajibu wa kisheria wa Israel kuruhusu misaada ya kibinadamu kufika kwa haraka kwa raia wa Palestina.

Israel pia inakabiliwa na tuhuma za kuzuia shirika la UNRWA la Umoja wa Mataifa, huku ikidaiwa kuzuia misaada kwa zaidi ya watu milioni 2.1 tangu Machi 2 mwaka huu.

SOMA: Wapalestina wagoma kuhamishwa GAZA

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button