Ubalozi Saudia watoa wito utuzaji wa fukwe

UBALOZI wa Ufalme wa Saudi Arabia Tanzania umetoa wito kwa jamii na wageni wanaotembelea fukwe za Mbezi kudumisha usafi wa mazingira na kushiriki katika kulinda eneo hilo la asili, ili libaki kuwa mfano wa mazingira safi yanayovutia watalii na jamii ya wenyeji.

Katika kuunga mkono Sera ya Mazingira na kuongeza uelewa wa jamii kuhusu umuhimu wa kulinda mazingira, Ubalozi huo umefadhili kampeni ya usafi wa ufukwe wa Mbezi, kwa kushirikiana na hilo Mtandao wa Afrika wa Haki za Binadamu (AHRN).

Balozi wa ufalme wa Saudi Arabia Tanzania, Yahya Ahmed Okeshi ametoa huyo jana Dar es Salaam na kueleza Ushirikiano huo ni kwa ajili ya kulinda mazingira ya baharini, kuimarisha uhifadhi na ukuaji wa viumbe hai na kusaidia juhudi za kuvutia utalii endelevu katika eneo hilo.

“Msaada huu ni mwendelezo wa mpango wa kitaifa wa kujitolea ulioanzishwa na Ufalme wa Saudi Arabia, na unatokana na juhudi za Wizara ya Mambo ya Nje za kusambaza maadili ya kazi ya kujitolea na kuimarisha ushirikiano na wadau wa ndani na wa kimataifa katika nyanja za za mazingira na jamii,”alisema Okeshi.

Pia alisisitiza umuhimu wa ushirikiano wa kimataifa na wa kijamii katika kulinda na kuhifadhi rasilimali za asili kwa vizazi vijavyo.

 

Aidha aliushukuru Mtandao wa Afrika wa Haki za Binadamu (AHRN) kwa kuonyesha juhudi katika kuandaa mpango huu.

“Shukrani zake kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira,) Mhandisi Hamad Y Masauni, kwa msaada na ushiriki wake wa katika kampeni, pamoja na wote waliojitolea na taasisi rasmi na za kijamii zilizochangia kufanikisha tukio hili,” alisema.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira,) Hamad Masauni amesema kasi ya uzalishaji taka nchini imeendelea kuongezeka hadi kufikia tani 20.7.

Amesema kutokana na ongezeko hilo, Serikali inalazimika kufanya mabadiliko ya sera ya mazingira pamoja na baadhi ya sheria ili kudhibiti uharibifu wa mazingira nchini.

Masauni amesema Serikali itahakikisha inaweka mipango na mkakati ya kukabiliana na ongezeko la hasa mijini kutokana na kasi kubwa ya uzalishaji wa taka hasa Dar es Salaam ambapo zinazalishwa taka asilimia 15.3.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button