Mpango maalum: Vijana Kagera washiriki uzalishaji kahawa

KAGERA: Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Fatma Mwassa amewasilisha mpango maalumu wa kuhakikisha vijana na wanawake mkoani Kagera wanashiriki kikamilifu kilimo cha zao la kahawa.

Lengo kuongeza uzalishaji wa zao hilo kutoka tani 60,000 zinazozalishwa kwa sasa hafi tani 200,000 ifikapo mwaka 2030

Aliwasilisha taarifa hiyi katika kikao cha wadau wa kahawa mkoani Kagera ambacho wadau wake wanajadili na kutambua fursa, changamoto zinazolikabiri zao la kahawa na jinsi ya kuongeza mavuno ambapo amepongeza msimu ulioisha 2024/2025 kwa kuingia zaidi ya Sh bilioni 250 kupitia zao hilo na halmashauri za mkoa wa Kagera kunufaika na Sh bilioni 7 kama mapato ya ndani.

Alisema kuwa ili kuongeza uzalishaji mkoa wa Kagera umetenga eneo la hekta 10,000 kwa ajili ya vijana nawanake ambapo kwa kuanzia wilaya ya Karagwe itapata hekta 2,000 na Wilaya ya Muleba hekta 2,000 na baaaye wilaya nyingine zitafuata kupewa maeneo kwa ajili ya kusaidia vijana kupata maeneo mapya ya kilimo.

Alisema mpaka sasa mkoa wa Kagera tayari umeanzisha shamba la mfano katika Kijiji cha Makongora wilayani Muleba na katika eneo hilo vijana na wanawake 300 kila mmoja amepata hekari moja iliyofungwa miundombinu yote kwa ajili ya kuitunza na kuisimamia ili baada ya muda mfupi waweze kuvuna kahawa na kuongeza kipato.

“Serikali imeongeza bei ya kahawa kutoka Sh 1,200 hadi 5,000 hii haijawai kutokea kutokana na udhubutu tayari serikali imetoa trekta 5 za kilimo ambazo zinasaidia kuandaa miundombinu na mashamba darasa ya vijana ambao badae wataongeza tija katika uzalishaji ,kwa sasa pesa ya kilimo cha kahawa Iko nje nje tujikite katika kilimo “alisema Mwassa.

Kupitia kikao hicho aliwaagiza wakurugenzi wa halmashauri zote na wakuu wa wilaya kuhakikisha wanasimamia asilimia 20 inayotokana na mapato ya kahawa inarudi kusaidia kilimo cha kahawa na kuzalisha miche yenye ubora huku akipiga uvunaji wa kahawa mbichi ambao unaharibu ubora wa zao la kahawa sokoni

Meneja wa Bodi ya Kahawa mkoani Kagera, Edmond Zani alisema kuwa uhitaji wa kahawa aina ya Robsta Katika nchi za nje kwenye masoko ni mkubwa sana hivyo jitihada za wananchi na wadau wote kuhamasisha kulima zaidi zaidi zao hilo zinahitaji huku aliwahakikishia wadau kuwa Kutokana na mipango iliyowekwa katika mkutano wa nchi 25 zinazolima kahawa Afrika bado bei ya kahawa itaendelea kuimarika katika masoko ya dunia.

Alisema kuwa kwa mwaka 2024/2025 malengo yalikuwa ni kukusanya tanu za Kahawa kutoka kwa wakulima wa mkoa wa Kagera 74.8 na Tani zilizokusanywa ni 54.2 sawa na asilimia 72.4 huku akidai kuwa jitihada zaidi za uzalishaji bado zinahitajika ili kuongeza pato la mkoa wa Kagera na uchumi wa mwananchi mmoja mmoja .

Alisema kuwa bodi ya kahawa inatarajia kushirikiana taasisi ya utafiti wa zao la kahawa TACRI kugawa miche bure kwa wakulima wa Kahawa 17,164,000 ili kuongeza uzalishaji ambapo alisema kuwa tayari bodi ya kahawa nchini imetangaza kufungua msimu wa ununuzi wa kahawa kwa bei ya shilingi 5,000 kwa kahawa ya maganda.

Alitaja changamoto zilizojitokeza katika msimu wa kahawa uliopita ni kuwa vyama vya msingi viliwasilisha kahawa hewa katika mnada na wanunuzi walivyofika katika vyama vyao walikuta mgahala hewa,utoroshaji wa kahawa ambayo inavunwa mapema kabla ya mnada kufunguliwa , uvunaji wa kahawa mbichi inayopoteza ubora pamoja na matumizi kidogo ya kahawa katika soko la ndani.

Alberth Katagira mmoja wa wazalishaji wa miche ya kahawa ameiomba serikali na Bodi ya Kahawa kufanya utafiti kwa wakulima wanaopewa Miche ya kahawa kama Miche hiyo kweli wanaisimamia inastawi au inakabiliwa na changamoto nyingine kuliko kuongeza Miche mipya Kila msimu bila kubaini changamoto za awali.

  • Aidha aliomba serikali kutoa elimu kubwa kwa wakulima wa mkoa wa Kagera Kuhusu matumizi ya mbolea kwani baadhi ya wakulima wanamawazo tofauti kuhusu matumizi ya mbolea inayotolewa kwa ruzuku na serikali kwa kuhofia kuwa itaharibu mashamba yao ya migomba.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button