Netanyahu awashutumu viongozi wa Ulaya kuhusu Gaza

TEL AVIV : WAZIRI Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, amewashutumu viongozi wa Uingereza, Ufaransa na Canada kwa kile alichokiita “kuwapa Hamas zawadi kubwa” baada ya kutoa wito wa kusitishwa kwa mashambulizi ya kijeshi Ukanda wa Gaza.

Kauli hiyo ya Netanyahu imekuja kufuatia tamko la pamoja lililotolewa Jumatatu na Waziri Mkuu wa Uingereza, Keir Starmer, Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron, na Waziri Mkuu wa Canada, Mark Carney, wakitaka Israel kusitisha operesheni zake za kijeshi na kuruhusu misaada ya kibinadamu Gaza.

Licha ya wito huo, Netanyahu amesema Israel itaendelea na mashambulizi hadi Hamas itakaposambaratishwa kikamilifu na mateka wake wote kuachiwa.

“Tangu mwanzo wa vita tulisisitiza kuwa ushindi kamili unapatikana kwa kuangamiza Hamas na kuwaokoa mateka wetu. Tutadhibiti kila sehemu ya Gaza hadi lengo hilo litimie,” alisema Netanyahu.

Hapo awali viongozi hao wa Magharibi walionya kuwa endapo Israel haitabadilisha mkakati wake, watakuwa tayari kuchukua hatua zaidi, huku wakisisitiza pia umuhimu wa Hamas kuwaachilia huru mateka waliotekwa tangu mashambulizi ya Oktoba 7, 2023.

SOMA: Bunge la Israel lapitisha sheria tata

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button