Wananchi wajitokeza kwa wingi uchunguzi magonjwa ya moyo

DAR ES SALAAM: WANANCHI zaidi ya 120 wamejitokeza kufanyiwa uchunguzi wa magonjwa ya moyo katika kambi ya siku mbili inayoendea kituo cha magonjwa ya moyo Kampasi ya Mloganzila, Dar es Salaam.

Kambi hiyo imeandaliwa na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili ( MUHAS ).

Akizungumza katika eneo hilo, Makamu Mkuu wa Chuo Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Appolinary Kamuhabwa amesema lengo la kambi hiyo ni kujua matatizo ya wananchi na kuwapa njia sahihi ya kupata matibabu.

“Tunatarajia idadi huenda ikaongezeka, tuna wataalamu wa kutosha, tuna wataalamu wa lishe pia,”

Prof Kamuhabwa alitaja sababu ya zoezi hilo kufanyika wiki hii ambapo alisema Ijumaa wiki hii watafungua kituo cha awamu ya pili cha umahiri wa magonjwa ya moyo na mishipa ya damu Afrika Mashariki sambamba na ujenzi wa jengo la magonjwa ya moyo ambapo mgeni rasmi atakuwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda.

SOMA ZAIDI: Muhas waandaa kambi uchunguzi magonjwa ya moyo

“Hiki kituo kikikamilika tutakuwa tumeweka miundombinu na mipango ya kuhudumia wananchi wa magonjwa ya moyo ambayo yanazidi kuongezeka,” alisema Prof Kamuhabwa.

Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa MUHAS, Profesa Emmanuel Balandya alisema kwa ajili ya kuboresha upasuaji wa moyo, MUHAS imeanzisha programu ya Master of Science and Cardiovascular Surgey lengo kuboresha eneo la usuaji wa moyo.

“Tangu tuanze kuzalisha na juhudi za Taasisi ya Jakaya Kikwete (JKCI) tunaanza kuanzisha wapasuaji wa moyo hapa hapa Tanzania, MUHAS kwa kushirikiana na JKCI,” alisema Prof Balandya.

Aidha ameongeza kuwa wameanza kuzalisha manesi ambao wamebobea katika kuwahudumia wagonjwa wa moyo.

“Juhudi zetu ni kuhakisha tunatoa wabobezi katika eneo la moyo,” amesema Prof Balandya,”

Hassan Riyami, mwananchi aliyejitokeza kufanya uchunguzi huo amesema kambi hiyo imesaidia kupunguza gharama kubwa ambazo wangetumia maeneo mengine kupata huduma hiyo.

Maria Tadei, kutoka mkoani Morogoro amesema amevutiwa na huduma hizo, kwani licha ya kuchunguzwa pia wamepokea ushauri wa kutosha kuhusu masuala ya moyo.

Mtemi Chitema Mahunguchira, kutoka  Mbagala,Dar es Salaam alisema:

  • “Nashukuru sana MUHAS kwa kuleta huduma hii karibu na wananchi. Wengi wetu hatujawahi kupima moyo kutokana na ukosefu wa elimu au hofu ya gharama. Hii ni hatua nzuri sana. Naomba programu kama hizi ziwe zinafanyika hata katika vituo vya afya vya wilaya.”

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button