Tamasha la elimu ya matumizi gesi asilia

SHIRIKA la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limeendesha bonanza kwa wanafunzi wa baadhi ya shule za sekondari mkoani Mtwara kwa lengo la kuendeleza uhusiano na ujirani mwema.

Akizungumza wakati wa bonanza hilo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano cha shirika hilo Marie Msellem amesema TPDC lengo ni pamoja na kuanzisha klabu za TPDC zinazotoa elimu juu ya namna nzuri ya matumizi ya gesi asilia.

Bonanza hilo limefanyika katika shule ya sekondari ya Mangamba iliyopo Manispaa ya Mtwara Mikindani likijumuisha michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa pete, kukimbia kwenye gunia, kufukuza kuku na mpira wa miguu huku shule za sekondari zilizoshiriki zikiwemo Msimbati, Naliendele, Mangamba na Ziwani.

Msellem amewahimiza wanafunzi hao kuwa mabalozi wazuri na walinzi wa miundombinu ya gesi asilia katika maeneo yanayowazunguka.

Katika bonanza hilo shule ya sekondari Ziwani imetwaa ubingwa wa mchezo wa mpira wa miguu kwa mikwaju minne ya penati dhidi ya tatu za Mangamba.

Baadhi ya wanafunzi wameishukuru TPDC kwa kuandaa mashindano kwani kupitia michezo kama hiyo husaidia kuibua vipaji mbalimbali kwa vijana.

WameSEMA  bonanza hilo limesaidia kuimarisha uhusiano mzuri baina ya shule moja na nyingine katika sekta ya michezo na taaluma hivyo wameiomba TPDC kuendeleza kuratibu michezo hiyo.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button