‘Tutapambana kuhakikisha mifumo hospitali isomane’

WAZIRI wa Afya Jenista Mhagama, amesema wizara yake itapambana kuhakikisha mifumo ya vipimo vinavyofanywa kwa wagonjwa visomane katika hospitali zote nchini.

Akifanya majumuisho kwenye hoja mbalimbali za wabunge waliochangia hotuba yake ya makadirio ya mapato na matumizi ya fedha ya Wizara ya Afya kwa mwaka 2025/2026, Waziri Mhagama amesema tayari wameanza na baadhi ya hospitali za Rufani za Mikoa na za Kanda na sasa wanaelekeza nguvu kwenye hospitali nyingine za chini.

Amesema haiwezekani mgonjwa anatoka Songea amepimwa, lakini akifika Njombe atatakiwa kupimwa upya kipimo kilekile na wakati mwingine kumuongezea gharama mgonjwa.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button