Mwenge kupitia miradi 75 ya Sh bil 28/- Tanga

TANGA: MWENGE wa Uhuru leo umeanza mbio zake mkoani Tanga ukitokea Dar es Salaam ambapo unatarajiwa kupitia miradi 75 yenye thamani ya Sh bilioni 28.6.

Akizungumza mara baada ya kupokea mwenge huo kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Dk Batlida Buriani amesema kuwa mwenge utakimbizwa katika halmashauri 11 zilizopo mkoani hapa.
“Ukiwa mkoani Tanga Mwenge wa Uhuru utaweza kuzindua miradi ,kuweka mawe ya msingi na kukagua miradi iliyopo kwenye sekta mbalimbali zilizopo kwenye wilaya nane za mkoa huu.




