Serikali itusaidie kuipaisha zaidi sekta ya utalii -Beatrice Dimitris

ARUSHA: BAADA ya Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kuifungua sekta ya utalii, wadau na wafanyabiashara wanaendelea kutumia fursa hiyo kukuza uchumi wa taifa na kuingiza fedha za kigeni.

Wakati watalii wakiendelea kumiminika na wengine kushuhudia kilele cha maonesho ya utalii ya Karibu -Killifair watalii wamekutana na manzigira mazuri ya sehemu za kulala na huduma muhimu baada ya Hotel ya Ngurdoto Mountain Lodge iliyopo Arumeru kuboresha na kuja kwa nguvu zote kutoa huduma hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha kwenye kilele cha maonesho ya utalii ya Karibu -Killifair ,Meneja wa hotel hiyo, Beatrice Dimitris Dallaris amesema sekta ya utalii nchini inazidi kukua kwa kasi sana na hii imetokana na jitihada za Samia Suluhu Hassan kuifungua nchi kupitia filamu ya The Royal Tour ambayo imeleta mafanikio makubwa.

“Nimefurahi sana kuona maonesho haya yameendelea kutanuka na kuwa makubwa sana kwani ata nchi nyingi za majirani zimeshiriki na watu mbalimbali wakionyesha bidhaa zaina zote zinazo tumika kwenye sekta hii ya utalii,”amesema Beatrice.

“Nimepewa nafasi ya kipekee kuja hapa nikimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Ngurdoto Mountain Lodge ‘Joan Auye Mrema na sisi kama Ngurdoto Mountain Lodge tunaangukia katika mhimili wa sekta hii ya utalii ambao kwa sasa imeleta sura mpya na mabadiliko makubwa sana na kuwa gumzo kila kona ya dunia,”amesema

“Sisi kama Ngurdoto Mountain Lodge tunapenda kunatoa shukrani za kipekee kwa Rais wetu, Samia Suluhu Hassan ambaye ameweza kutupia jicho la pili kwenye sekta ya utalii na sasa tumeamka na kuanza tunafanya vizuri, kwa pamoja tutaendelea kuunga juhudi zake katika kukuza na kuendeleza utalii kwa kuhakikisha sekta ya utalii haipoi inasonga mbele na kuendelea kuvutia wenyeji, majirani na watalii zaidi,” amesema .

Beatrice ameongeza kwa kusema lengo la kuu la kutembelea maonesho hayo ni kukutana na wadau wa sekta ya utalii na huduma nyingine kupata fursa ya kuitangaza upya hotel hiyo kwa wananchi pamoja na wadau wa utalii,” amesema.

Ameongeza: “Hivi karibuni wameweza kupata baraka ya kuweza kuhudumia Gala Dinner ya TAA-ACI AFRICA 2025, sio ivyo tu walipata nafasi ya kipekee ya kuhudumia mkutano mkubwa wa chama cha waendesha Ofisi za Serikali TAPSEA uliokuwa na washiriki zaidi ya elfu tano ambapo baadhi yao waliweza pia kuhudumiwa ya malazi, na kupata huduma ya usafiri kutoka wiwanja vya ndege na kuweza kutembelea vivutio mbalimbali kupitia kampuni yao ya utalii”.

Ameongeza kuwa kama mdau wa utalii anaipenda sana sekta hiyo kwani ambayo ameifanyia kazi kwa zaidi ya miaka 18 sasa na amepata uzoefu ndani ya sekta hiyo kiujumla, aneongeza kwa kusema bado hajachoka kujifunza.

Aidha, ameiomba serikali kuendelea kuwaangalia na kuwasaidia katika kuhakikisha sekta hiyo inazidi kupaa zaidi ili watu kuweza kunufaika na fursa mbalimbali zilizopo na zijazo kwenye nchi yetu.

“Nawakaribisha watanzania wote kwa ujumla, nchi za majirani na dunia kwa ujumla kwani Ngurdoto Mountain Lodge ipo na ina bei za kawaida sana kuanzia malazi ya vyumba aina mbali mbali venye uwezo wa kulaza watu 394 kwa mara moja na miongoni ni presidential villa ambazo zipo 15 na pia kuna vivutio vingi kama viwanja vya michezo mbalimbali , bwawa la kuogelea kwa wakubwa na watoto, michezo ya watoto na sehemu ya mazoezi.”

Aidha amewataka wadau kuutumia ukumbi wao wa kimataifa kwa shughuli zao mbali mbali kwani ukumbi wao una uwezo wa kuchukua watu wengi kufikia elfu nane wakiwa wamekaa wote na ndani ya ukumbi na sehemu ya kula chakula wakiwa wamekaa kwa kiwango hicho hicho.”amesema .

Ameongeza kuwa ,wana kumbi zingine ambazo zinaweza kuchukua watu mia tano, mia nne , na nyingine ambazo zina uwezo wa kuchukua watu mia moja na nyingine ndogondogo.

“Tunashukuru sana kwamba watu wameendelea kutuunga mkono na kutufanya hoteli yetu ya Ngurdoto Mountain Lodge kuendelea kusonga mbele na inatuwezesha na sisi kuendelea kuunga mkono na kwa pamoja tuzidi kukuza sekta yetu ya utalii ili izidi kuwa bora zaidi na kupaa zaidi na zaidi .”amesema .

Ameongeza kuwa, kutoka uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro hadi kufika hotel ya Ngurdoto Mountain ni kilometa 27 tu na kutoka Arusha Mjini pia ni kilometa hizo hizo 27, ambapo kutoka hotelini hapo hadi hifadhi ya Arusha ni kilometa 7.5 .

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button